Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Haruna Lipumba |
Chama cha wananchi Tanzania CUF kimeshauri kwamba
kuna umuhimu wa serikali TATU katika katiba mpya itakayoundwa ili kuondoa
migongano na kero za Muungano.
Akiongea mara baada ya kutoa maoni yao kwa tume ya
katiba,Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Haruna Lipumba amesema kuwa amesema
muundo wa serikali tatu utalifaa taifa la Tanzania,amezitaja serikali hizo kuwa
ni pamoja na serikali ya Tanganyika,Zanzibar na Muungano.
Profesa Lipumba amesema kuwa kumekuwepo na
Malalamiko hasa kutoka upande wa Zanzibar kuwa serikali ya Tanganyika imemezwa nay
a Muungano kutokana na muundo wa sasa.
Aidha katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo
amesema suala la rasilimali za nchi hiii zinatakiwa ziwekwe kikatiba ili kila
mwananchi aweze kufaidi matunda ya Uhuru wa nchi hii.
Masuala mengine yaliyopendekezwa na chama hicho
kwa tume ya katiba ni pamoja na suala la uteuzi wa viongozi, usawa wa kijinsia,maadili
ya viongozi na kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi ili kutoa fursa sawa ya kidemokrasa
katika siasa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment