Waziri Wa mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Emmanuel Nchimbi akizungumza jambo |
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi
kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za mtu ama kikundi cha watu
wanaosadikiwa kujihusisha na umiliki wa silaha isivyo halali au matukio ya
uhalifu wa aina yoyote ile.
Aidha, Mtu yeyote atakayetoa taarifa za mafanikio
zitakazowezesha kukamatwa kwa watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria
atazawadiwa kiasi cha shilingi laki moja (100,000/-) au zaidi kulingana na mafanikio
ya taarifa aliyoitoa.
Kutokana
na tatizo la kuzagaa na matumizi holela ya silaha zinazomilikiwa
isivyo halali na kinyume cha sheria hapa nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi Mheshimiwa DKT Emmanuel Nchimbi (Mb), alitoa wito katika kipindi cha
mwezi mmoja kwa mtu yeyote ama kikundi chochote kinachomiliki silaha kinyume
cha sheria na isivyo halali kusalimisha silaha hizo katika vituo vya
polisi vilivyo karibu yao au ofisi za serikali, wenyeviti wa vitongoji,
kata, serikali za mitaa, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na taasisi za kidini. Zoezi hili limefanyika kote nchini kuanzia Desemba 3, 2012 hadi Januari 4, 2013. Aidha, Mhe. Waziri Nchimbi alisisitiza kuwa, katika kipindi hicho cha msamaha hapatakuwa na hatua zozote za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayesalimisha silaha kwa hiari. Pale ambapo silaha hiyo itakuwa imesalimishwa msalimishaji hatabughudhiwa kwa namna yoyote ile, jambo ambalo limefanyika kwa mafanikio makubwa.
Aidha, katika zoezi hilo, jumla ya silaha 439 zimesalimishwa na Risasi 37. Miongoni mwa silaha zilizosalimishwa na idadi yake katika mabano ni pamoja na Shortgun (29), Gobore (352), SMG (11), Riffle (20), Pistol (22), Airgun (1), Rocket launcher (2) na SAR (2). Tunawapongeza wote waliotoa ushirikiano kwa kusalimisha silaha hizo kwa hiari.
Baada ya muda wa msamaha kuisha, Jeshi la Polisi tayari limejipanga kwa oparesheni maalum inayoendeshwa nchi nzima kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola pamoja na raia wema ili kuweza kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria ama waliokaidi kuzisalimisha silaha hizo kwa hiari yao ili sheria iweze kuchukua mkondo wake. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment