Mwenyekiti BAVICHA Taifa Ndugu John Heche
Kamati tendaji ya baraza la vijana la Chama cha demokrasia na maendeleo BAVICHA limewafuta uanachama,wanachama wake sita wakiwemo baadhi ya viongozi waandamizi wa baraza la hilo.

Akitangaza uamuzi huo,mwenyekiti wa BAVICHA Taifa,John Heche amesema wanachama hao akiwemo makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Juliana Shonza wamefukuzwa kutokana na makosa mbalimbali ambayo kila mmoja wao aliyatenda kwa nyakati tofauti.

Ameyataja makosa hayo kuwa ni pamoja na kusema uongo dhidi ya viongozi wa juu wa chadema na kusababisha mivutano yenye kulenga kuvuruga chama
Amewataja wengine waliofukuzwa kuwa ni  katibu wa BAVICHA mkoa wa Mwanza Ben Saanani ambaye anatuhumiwa kuwatusi wananchama wenzake kupitia mtandao.
Wengine waliofukuzwa ni aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mtera Mwampamba na mwenzake Habib Mchange, aliyekuwa anawania ubunge jimbo la Kibaha mjini

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa kamati tendaji pia imewaandikia barua za onyo na kuwaweka kwenye kipindi cha uangalizi baadhi ya wananchama ambao pia wamekiri kufanya vitendo vinavyoweza kukivuruga chama na kufafanua kuwa hatua hizo ni kwa mujibu wa katiba ya Chadema. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top