Rais Mtaafu wa Zanzibar Dk Aman Abeid Karume akitoa hotuba ya kufungua shule ya Donge Muwanda Kaskazini Unguja katika shamrashamra za kuazimisha miaka 49 ya mapinduzi ya Zanzibar. |
Rais mstaafu awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzíbar Dkt. Amani Abeid Karume amewataka Wanafunzi wa Skuli ya
Sekondari Muwanda kutumia muda wao mwingi katika masomo ya Sayansi ili kupata Wataalamu
wa masomo hayo watakaoendana na maendeleo ya kisasa.
Dkt. Karume ameyasema hayo huko Donge Muwanda wakati wa
ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Donge ikiwa ni shamra shamra za sherehe ya
kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzíbar.
Amesema Wanafunzi hao wanapaswa kuyapa kipaumbele masomo
hayo kwa vile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzíbar imegharamika kuleta Walimu wa
masomo ya Sayansi kutoka Nchini Nageria na Skuli hiyo kubahatika kupata
Walimu hao.
Amewataka wanafunzi hao kutumia fursa hiyo kushirikiana
na wataalamu waliopo ili waweze kufaulu mitihani yao na hatimaye kujiunga na Vyuo
vikuu kupitia masomo ya Sayansi.
Dkt. Karume pia amewataka wazazi na wanakamati wa Skuli
hiyo kuwahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii huku Waziri wa Elimu ambaye pia ni
Mwakilishi wa Jimbo la Donge Ali Juma Shamhuna akiahidi kuifanya Skuli hiyo kuwa ya masomo ya sayansi kwa Wilaya
nzima
(PICHA NA YUSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR) TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment