JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetaja shule 24 za sekondari ambazo zitatoa wanafunzi elfu 5 watakaomaliza kidato cha sita na kujiunga na jeshi hilo. Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Raphael Mahuga imesema kuwa wanafunzi hao watatakiwa kujiunga na jeshi hilo ifikapo
Machi 2, mwaka huu.
Shule hizo za sekondari ni Kibondo, Musoma, Kibaha, Ilboru, Bagamoyo, Jitegemee, Tabora Wavulana na Nganza.Shule nyingine ni Mtwara Wasichana, Ihungo, Kilakala, Benjamin Mkapa, Maswa Wasichana, Dodoma, Tumain-Singida na Galanos. Nyingine ni Ashira, Nangwa-Manyara, Iyunga, Mpanda, Lindi, Iringa Wasichana, Kawawa-Iringa na Ruhuwiko-Songea.
Taarifa hiyo meongezaza kuwa maofisa wa JKT watakwenda kwenye shule hizo kuanzia Januari 9, mwaka huu kwa ajili ya kutoa utaratibu wa mafunzo na kambi ambazo watakwenda. Hatua hiyo ni kulingana na sheria ya mwaka 1964 na kufanyiwa mapitio mwaka 2002, chini ya kifungu cha sheria namba 5,na inaanza kutekelezwa tena tangu iliposimamishwa mwaka 1994.
Kwa mujibu wa jarida la JKT, mafunzo hayo ya miezi sita yatatolewa katika Kambi za JKT Bulombora na Kanembwa mkoani Kigoma, Mlale mkoani Ruvuma, Mafinga mkoani Iringa, Msange mkoani Tabora na Oljoromkoani Arusha. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment