Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia sera na uratibu, William Lukuvi.
Tume ilioundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuchunguza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana, LEO imeitaka serikali ifute matokeo yote na mitihani isahihishwe upya.
Akisoma ripoti ya Tume hiyo bungeni Mjini Dodoma LEO, Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia sera na uratibu, William Lukuvi amesema kwamba mitihani hiyo inapaswa kusahihishiwa kwa kuzingatia vigezo vilivyotumika katika kusahihisha mitihani ya kidato cha nne mwaka 2011.
Mwaka jana matokeo ya wanafunzi wa kidato cha nne yalikuwa mabaya kuliko matokeo mengine yaliowahi kutolewa na Baraza la Mitihani la Taifa. Wanafunzi walifeli kwa zaidi ya asililimia 60.
Kutokana na matokeo ya tume hiyo, Lukuvi ameipongeza tume hiyo kwa kutoa matokeo hayo.
Wataalamu wa elimu wanasema kwamba endapo serikali itatekeleza pendekezo hilo itaingia kwenye gharama kubwa ambazo pengine zitaigharimu serikali.
Wakati wadau wa elimu wakitafakari hayo chama cha walimu Tanzania CWT kimesema kinataraji kutoa tamko lake wiki ijayo kuhusiana na uamuzi huo ambao huenda ukaibua maswali mengi kuliko majibu.
Kaimu katibu mkuu wa chama cha Walimu Tanzania, Ezekiel Oluoch amesema kuwa hategemei jipya kwani matokeo yale hata kama yatarekebishwa bado ukweli haufichiki kuwa kuna changamoto kubwa zinazotakiwa kushughulikiwa kwa umakini zaidi badala ya kutumia njia za mkato.
0 comments:
Post a Comment