Mtandao wa jinsia Tanzania umependekeza katiba mpya itokane na mchakato utakaoshirikisha  sauti za wanawake na wanaume, na kuweka bayana  makubaliano ya  misingi mikuu itakayoongoza nchi
Mapendekezo hayo zaidi ya 20 ambayo mtandao huo umepeleka kwenye tume ya maoni ya katiba,na nakala yake kupatikana jijini,imeyataja mambo mengine ya kuzingatia kuwa ni kuendelezwa kwa haki za msingi zilizoko kwenye katiba ya sasa kwa kupinga vitendo vyote vya ubaguzi wa aina yoyote uliyojikita katika  jinsia, hali, rangi, dini au ukabila
Pia mtandao huo umependekeza mikataba kuhusu haki za wanawake na watoto ziwe sheria mara tu Tanzania inaporidhia huku pia wakitaka katiba Mpya  itoe mwongozo utakaobatilisha sheria  zote Kandamizi:
Katika maoni hayo pia mtandao wa jinsia umependekeza kuwepo kwa haki sawa za Uraia, Kulinda Utu wa Mwanamke,  haki ya kumiliki  Rasilimali za Nchi na haki za wanawake  kufikia na Kunufaika na huduma za msingi za Kijamii
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top