Abdul Quader Mollah
Mahakama ya Juu nchini Bangladesh imemhukumu kifo
mwanasiasa wa kiislamu aliyepatikana na hatia ya mauaji ya halaiki
wakati wa vita vya Ukombozi kutoka kwa Pakistan mwaka 1971.
Abdul Quader Mollah wa chama cha upinzani cha
Jamaat E Islami alihukumiwa maisha na mahakama maalum ya uhalifu wa
kivita hapo mwezi Fabruari.
Wakili wake amesema hii ndio mara ya kwanza hukumu ya maisha imeongezwa na kua kunyongwa.
Hukumu ya awali ilichochea maandamano ya wafuasi wa chama chake ambao wamesema hukumu dhidi ya Mollah imechochewa kisiasa ingawa wapinzani wake wanasema kuwa hukumu hiyo ni dhaifu mno.
Maelfu walifanya maandamano kote nchini wakitaka
Mullah ambaye alipatikana na hatia ya kuongoza mauaji ya halaiki wakati
wa vita vibaya zaidi vya kupigania uhuru anyongwe.
Maandamano hayo yalichochea bunge kufanya
mageuzi ya sheria ambayo yanaruhusu serikali kukata rufaa dhidi ya
uamuzi wowote ulioafikiwa na mahakama maalum ya uhalifu wa kivita nchini
humo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment