Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari Tanzania MOAT, Bwana Reginald Mengi
WAMILIKI wa Televisheni wameitaka serikali kurejesha matangazo ya mfumo wa analojia kutokana na mfumo mpya wa dijitali kukabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo wananchi kushindwa kumudu gharama zake.
Mwenyekiti wa wamiliki wa wa vyombo vya habari Tanzania MOAT Bwana Reginald Mengi amesema kuwa mfumo wa dijitali una mapungufu makubwa hivyo unatakiwa kwenda sanjari na analojia mpaka hapo matatizo yatakapofanyiwa kazi.
Bwana Mengi amesema kwa sasa televisheni zimekuwa zikiendeshwa kwa hasara kutokana na matangazo ya biashara kupungua katika vituo hivyo kwani imebainika kuwa wananchi wengi hawana ving’amuzi hivyo hawapati matangazo.
Athari nyingine iliyotajwa ni baadhi ya makampuni kuanza kupunguza wafanyakazi kutokana na mapato kupungua kwa mapato katika vituo vya Televisheni.
Kwa mujibu wa taarifa za utafiti zilizotolewa hivi karibuni na kituo cha taarifa kwa wananchi zinaonesha kuwa ni asilimia 25 tu ndiyo wanafuatilia matangazo ya televisheni huku asilimia 75 wakiwa hawana uwezo wa kupata matangazo husika.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment