MKE wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda amewataka akinamama wanaojihusishana shughuli za ujasiriamali kuwa waaminifu kwa wenza wao na wanafamilia wao ili waweze kupata ushirikiano kutoka kwao.

Amesema mbali ya majukumu mengi yanayowakabili, akinamama wanapaswa kuwa karibu na familia zao kwani ndiyo msingi mkuu wa Taifa amesema hawana budi kutoa malezi mema kwa wenza wao na familia kwa ujumla.

 Mama Tunu Pinda amesema wanawake wanapofanikiwa katika shughuli zao, wasiache kuwa waaminifu kwa wana-familia waheshimu na kuwaenzi kwa kuwashirikisha kazi wanazofanya ili waweze kupata ushirikiano wao na baraka zao.

Amesema akinamama wanapaswa kuungana kwenye vikundi vya ujasiriamali ili waweze kuunganisha ujuzi, stadi walizonazo na kushirikishana uzoefu. Alisema hawana budi kuhakikisha kuwa bidhaa wanazozalisha zinakuwa na ubora wa kiwango cha juu ili waweze kukabiliana na ushindani kwenye soko.


Amesema jamii haina budi kuwekeza zaidi kwa wasichana kwa kuwapa fursa za kujiendesha kibiashara pamoja na ujuzi (skills) ili waweze kujiajiri kwani wanakumbana na vikwazo vingi wanapotafuta ajira
ikiwemo, unyanyasaji na unyanyapaa
. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top