Imeelezwa kuwa udhibiti wa usafiri wa nchi kavu utawezekana endapo kutakuwa na mfumo bora wa mabasi machache  yenye viwango vya ubora wa hali ya juu.

Kaimu mkurugenzi wa Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu SUMATRA Ahmad Kilima amesema hali hiyo itawasaidia wafanyabiashara kufanya biashara kwa weledi na ufanisi na mamlaka kufanya kazi kwa viwango kwani inasimamia wadau wachache.

Mkurugenzi huyo amesema wanaweza kusisitiza suala la uchache wa kampuni za mabasi yaendayo haraka (DART) lakini lazima yawe na viwango vinavyolingana na mradi huo utakaokamilika  mwaka 2015.

Bwana Kilima amewataka wamiliki wa mabasi kujiunga katika ushirika ili kuendesha biashara ya usafiri kwa pamoja kwa kuimarisha huduma zenye tija zaidi kwa watumiaji.

Naye mwenyekiti wa wamiliki wa mabasi jijini humo DACOBOA Sabri Mabruki amesema suala la mabasi yaendayo haraka linatakiwa kuchukuliwa kwa umakini mkubwa vinginevyo linaweza kuleta athari katika jamii.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top