Jaji mstaafu Mark Bomani.
Baraza la habari Tanzania (MCT) limezindua kongamano kuhusiana na wajibu wa
vyombo vya habari katika kupambana na kauli za chuki na itikadi kali.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa MCT, Jaji mstaafu Mark Bomani amesema Mwandishi wa habari ana nafasi kubwa katika jamii
ambayo mara zote imekuwa ikijenga imani juu ya taarifa anazotoa.
Mbali na kufikisha taarifa Jaji Bomani amesema ni jukumu la waandishi wa habari kukemea na
kufichua maovu na kuhubiri amani katika jamii na kuonesha njia ya uwajibikaji.
Jaji Bomani pia amewataka waandishi wa habari
kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, maadili na weledi ili kujenga taswira yenye heshima na
uaminifu katika jamii.
MCT yazindua kitabu
Katika kuisadia sekta ya habari nchini, MCT imezindua kitabu ambacho kinatoa miongozo mbalimbali katika
tasnia hii ya habari ikiwamo maadili.
Vyombo vya habari vimetakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwapasha habari
wananchi habari mbali mbali licha ya changamoto kadhaa wanazokutana nazo wakiwa kazini .
Katibu mtendaji wa baraza la habari Tanzania MCT Bwana Kajubi mkajanga amesema Waandishi wa habari wamejitahidi
kufanya kazi kwa bidii licha ya mazingira magumu yanayorudisha nyuma utendaji wa
kazi zao .
Misingi ya awali ya Uwajibikaji wa waandishi wa
habari ujumbe kwa jamii ikiwa na lengo
la kuelimisha,kukosoa na kuunganisha jamii katika masuala mbalimbali ya
kiuchumi na kijamii.
Pia Katibu huyo amesema Waziri mkuu Mizengo Pinda
hakupaswa kuongea maneno yenye kutisha na kuchochea askari kuwakandamiza raia
bali angejikita zaidi katika kuhamasisha wananchi kutii sheria bila shuruti.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment