Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA,Dakta Willibroad Slaa
Suala la ubora wa mitaala ya elimu linazidi kuwa katika mjadala mkubwa hasa baada ya mbunge wa kuteuliwa James Mbatia kuanika udhaifu wa mfumo wa elimu hapa nchini.
Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA,Dakta Willibroad Slaa amesema amefuatilia na kugundua kuwa vitabu
vinavyotumika mashuleni vina udhaifu mkubwa kitaaluma na kitaalam.
Dakta Slaa amesema kitendo cha vitabu kuuzwa
kiholela kinadidimiza elimu ya Tanzania kwani watunzi,wahakiki na wasambazaji
wanaonekana kutokuwa na umakini suala la kufuatilia masuala ya elimu.
Aidha Dakta Slaa amekosoa kile kinachoendelea
katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kupoteza mwelekeo kwa
viongozi wa bunge na wabunge wenyewe.
Katibu huyo amesema kwa mujibu wa sheria na kanuni
za bunge kipindi hiki badala ya wabunge kulumbana kwa hoja binafsi ilitakiwa
kupelekwa miswada ya kutunga sheria.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment