Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano Anne Makinda amewataka wabunge kufuata sheria na kanuni za bunge ili kuwatendea haki wananchi waliowachagua.
Spika huyo amesema kuwa kitendo cha wabunge
kukiuka maadili kinawafanya wananchi kushindwa kuwaelewa kwani wanalumbana
kwa vitu ambavyo havina tija kwao.
Hata hivyo wakati akitoa maelekezo hayo kwa
wabunge walikuwa wakipiga kelele kuashiri kutounga ufafanuzi huo.
Katika vikao vya jana na leo vimeonesha wabunge
wengi kutofuata maelekezo ya spika na naibu wake kwa madai ya kutotendewa haki
hasa kwa vyama vya upinzani na kulazimika kuahirishwa kwa vikao hivyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment