Mkurugenzi wa kituo cha taarifa kwa wananchi TCIB, Deus Kibamba
Wanaharakati wametoa wito kwa watu wa Wizara ya
mawasiliano Tanzania kusitisha suala la kuzima mitambo ya analogia nchi nzima hadi hapo dosari mbalimbali za
mfumo wa dijitali zitakaporekebishwa.
Mkurugenzi wa kituo cha taarifa kwa wananchi TCIB Deus Kibamba amesema kuwa wizara ya
mawasiliano na taasisi zilizo chini yake hazikujipanga ndiyo chanzo cha
matangazo kurushwa katika viwango duni na kukatika mara kwa mara.
Bwana Kibamba amesema kutokana na usumbufu uliojitokeza kiuchumi na kijamii
serikali na mamlaka ya mawasiliano Tanzania inatakiwa kugharamia hasara kwa wamiliki luninga na wananchi.
Kituo cha TCIB kimegundua kupungua kwa watazamaji
kwa wananchi wengi wanashindwa kumudu gharama za kulipia ving’amuzi na
vifurushi vya chaneli mbalimbali.
Utafiti unaonesha kuwa tangu kuzimwa kwa mitambo
ya analojia jijini Dar es Salaam hapo Desemba 31 upatikanaji wa taarifa
umezorota kwa asilimia 70 na hiyo ni pamoja na mikoa mingine inayotegemea mkoa
huo kama chanzo kikuu cha taarifa.
Utafiti huo unaonesha kuwa kuna hatari ya baadhi
ya vituo kufa kabisa na hivyo kurejesha ukiritimba na umangimeza kwa vituo
vikubwa kutawala Nyanja ya habari mawasiliano.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment