WILAYA YA CHUNYA – ASKARI POLISI MMOJA AUAWA KATIKA MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI NA MAJAMBAZI


 MNAMO TAREHE 06.02.2013 MAJIRA SAA 00:30HRS HUKO  KATIKA HOSPITALI YA MWAMBANI – MKWAJUNI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA . ASKARI POLISI G.68 PC JAFARI KARUME MOHAMED MIAKA 30,MUHA WA KITUO CHA POLISI MKWAJUNI   ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO . CHANZO CHA TUKIO NI MAJAMBAZI  WANNE WAKIWA NA SILAHA  IDHANIWAYO KUWA AINA YA SMG WALIVAMIA KITUO CHA MAFUTA KILICHOPO KIJIJI CHA MATUNDASI MALI YA SAMORA S/O MUYOMBE NA KUPORA PESA TSHS 2,200,000/=  WAKITUMIA GARI T.227 BST AINA YA TOYOTA COROLA ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA SHABAN S/O MSULE,MIAKA 33,MBENA MKAZI WA MAKAMBAKO .MAREHEMU AKIWA DORIA NA ASKARI WENZAKE WALIFUATILIA TUKIO HILO NA KATIKA MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI ASKARI HUYO ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA RISASI UBAVU WA KULIA NA KUKIMBIZWA HOSPITALINI KWA MATIBABU ZAIDI . KATIKA TUKIO HILO JAMBAZI SHABAN S/O MSULE ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI .GARI  LILILOTUMIKA KATIKA TUKIO HILO LIMEKAMATWA NA MAGANDA 9 YA RISASI AINA YA SMG/SAR NA RISASI 6 ZIMEOKOTWA ENEO LA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU ASKARI G.68 PC JAFARI KARUME MOHAMED UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO .MSAKO MKALI UNAENDELEA CHINI YA UONGOZI WA RCO MBEYA ROBERT MAYALA – SSP,   ASKARI  POLISI NA WANANCHI ILI KUWABAINI NA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI .KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI  ANATOA WITO KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE , VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.       


                                                       [  BARAKAEL MASAKI – SSP ]
                                  KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top