Watu wasiojulikana wameteketeza
nyumba saba katika eneo la kuhifadhi wanyama mjini Lamu , ingawa hakuna
vifo vimeripotiwa katika shambulizi la hivi karibuni.
Washambuliaji walifanya uharibifu mkubwa kwa kuteketeza magari na ofisi
Takriban familia 500 zinatoroka na
kukimbilia usalama wao katika maeneo jirani ambako mashambulizi mengine
mawili yalitokea mjini Lamu na katika eneo la Tana Delta na kusababisha
vifo vya watu 29 mwishoni mwa wiki.
Chanzo cha familia hizi kuanza kutoroka makwao kabla hata ya kuwazika jamaa zao, ni swala linalowatia wasiwasi maafisa wakuu.
Wengi walilazimika kulala nje ya gereza la Hindi baada ya kutoroka mashamba yao.
Familia nyingi pia zimepiga kambi nje ya lango kuu la Kambi ya jeshi iliyo karibu na eneo hilo.
Wengi wanahisi kuwa salama katika kambi hizi kinyume na hali ilivyo nyumbani kwao.
Msemaji wa shirika la Red Cross,Waita Wariko, aliambia BBC kuwa watu wengi wameshuhudiwa wakihama makwao kutafuta maeneo salama.
Licha ya hali hiyo, watu hao wameombwa kurejea makwao, lakini hawana imani na polisi hususan kuhusu usalama wao.
Makamu wa Rais William Ruto, aliyezuru eneo hilo
Jumapili, alitoa makataa ya saa 48 kwa maafisa wakuu wa usalama
kuwasaka washambuliaji , wakiwa hai au wafu la sivyo, wafutwe kazi.
Hakuna mshukiwa hata mmoja amekamatwa mpaka sasa.
Mauaji hayo yamesemekana kuchochewa na swala
tete la umliki wa mashamba na kuna wasiwasi wa kutokea mashambulizi ya
kulipiza kisasi kutoka kwa jamii moja ambayo watu wake wengi
walishambuliwa hivi karibuni.
BBC
0 comments:
Post a Comment