Watu watatu wamefariki na
wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa wakati gereza moja lilipoteketea kwa moto
magharibi mwa Rwanda, karibu na mpaka wa DRC.
Tukio hili linatokea mwezi mmoja baada ya gereza jengine, Muhanga, kuteketea kwa moto katika jimbo lililopo kusini mwa Rwanda.
Ajali hiyo ya moto imeripotiwa
kutokea majira ya jioni (Jumatatu) katika gereza la Nyakiriba, katika
wilaya ya Rubavu mpakani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
'Uokozi haukutosha'
Akiongea na BBC kwa njia ya simu mkuu wa wilaya
hiyo, Sheikh Hassan Bahame, amesema kuwa juhudi za uokozi zimefanyika
haraka ila mahabusu 3 walifariki na wengine 44 kupatwa na majeraha ya
moto.
Majeruhi walifikishwa mara moja katika hospitali kuu ya wilaya.
Amesema kuwa kutokana mazingira ya milima ambapo
gereza hilo limejengwa, imekuwa vigumu kwa wazima moto kufanya kazi yao
kwa wepesi na haraka.
Shekh Bhame ameelezea hasara iliyojitokeza.''
Hasara kubwa abayo imetokea ni kifo cha hawa wafungwa. Na majeraha
waliyopata wafungwa wengine. Kuna vitu vingi vimeharibika na hatujajua
idadi yake bado.''
Sheikh Bahame ametahadharisha kuelekeza lawama
la shambulio la kigaidi akisema kuwa japo inatia shaka, ni muhimu
uchunguzi zaidi kufanywa.
''Hata sisi tunajiuliza, mbona mambo haya
yametokea, na juzi tu yametokea Muhanga?Inatakiwa uchunguzi wa ndani
zaidi ufanywe. Lakini uhakika bado hatujapata.'' Amesema Sheikh Bahame.
Uchunguzi umeanzisha kujua chanzo cha moto, pamoja na ule moto katika gereza la Muhanga mwezi mmoja uliopita.
BBC
0 comments:
Post a Comment