Kikosi cha Timu ya Taifa Nigeria (The Super Eagles)

Sunday Mba
HATIMAYE timu ya taifa ya Super Eagles imefanikiwa kutwaa kombe la mataifa huru ya Afrika (AFCON)-2013, walilolikosa kwa miaka 19, kwa kuifunga timu ya Burkina Faso bao 1-0.

Mchezo ulianza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kufanya mashambulizi ya kushitukiza jambo lililowafanya Wanigeria wasubiri hadi dakika ya arobaini ndipo Sunday Mba alifunga goli baada ya kutokea kizaazaa langoni mwa Wabukinabe. Hadi dakika arobaini na tano za kwanza zinaisha matokeo yalibaki 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Burkina Faso kucheza kwa kutulia jambo lilionekana kuwapa shida Super Eagles.

 Dakika za mwishoni Burkina Faso walianza kucheza pasi ndefu kuelekea langoni mwa Super Eagles jambo lililofanya mchezo kupunguza ladha ya mwanzo.

Katika mchezo huo wachezaji watano wa Super Eagles walioneshwa kadi za njano wakati mchezaji mmoja wa Burkina Faso alioneshwa kadi hiyo.

Hadi dakika ya tisini matokea yalibaki 1-0 na kuwafanya Super Eagles watawazwe kuwa mabingwa wapya wa Kombe la AFCON 2013 ambalo lilikuwa linashikiliwa na Timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo) iliyoondolewa katika hatua ya makundi.

Nafasi ya tatu imechukuliwa na timu ya Mali baada ya kuilaza timu ya Ghana kwa jumla ya bao 3-1 katika mchezo uliochezwa juzi Jumamosi kwenye uwanja wa Nelson Mandela.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top