Spika wa Bunge, Anne Makinda

 Uongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umesema  spika  na naibu spika wa bunge  wameshindwa kufanya kazi kwani nafasi hiyo haiwatendei haki wananchi

Mkurugenzi  wa oganaizesheni na mafunzo wa chama hicho  Beson Kigaila amesema kuwa yanayotokea bungeni mjini Dodoma ni matokeo ya kiti cha spika kinachoongozwa na Anne Makinda na naibu wake Jobu Ndugai kutokuzingatia kanuni za bunge ambazo wamezitunga wenyewe.


Bwana Kigaila amesema wao  chadema wanaamini  kuwa bunge ni sauti ya wanyonge na wanachi kwa ujumla hivyo wanawataka  viongozi hao wa bunge kufanya kazi bila upendeleo kwani wabunge wote ni wawakilishi wa wananchi

spika Makinda na naibu wake Job Ndugai kama sio kutojua kanuni za bunge basi wanaleta ushabiki wa chama mahali ambapo sio penyewe na kutaka kupotosha umma kuwa chadema kinasababisha vurugu ndani ya bunge na sio kweli.’alisema kiongozi huyo.


Hivi karibuni kulijitokeza hali ya mgogoro wakati wa kujadili hoja binafsi za wabunge na kusababisha Spika kusitisha uwasilishaji wa hoja binafsi  zote hatua ambayo imesababisha mgongano wa mawazo katika jamii kuhusu hatua hiyo.


Katika hatua nyingine kiongozi huyo amesema  wamejipanga kwaajili ya kuwapokea wabunge wote wa kambi ya upinzani na baadaye mkutano mkubwa utakao fanyika Temeke Jumapili wiki hii.


Kigaila ambaye pia ni mratibu wa maandamano hayo amesisitiza kuwa chama chake na upinzani kwa ujumla kinataka wananchi ambao ndio wenye dhamana na wabunge waamuwe ikiwa spika na naibu wake wanafaa kuliendesha bunge au la.

Kigaila amezidi kuongeza kuwa mwenye mamlaka ya kuondoa au kerekebisha hoja aliyoiwasilisha ni mbunge mwenyewe lakini inashangaza kuona hoja za msingi za wabunge James mbatia NCCR-MAGUZI na John Mnyika CHADEMA zilivyo ondolewa kinyume na kanuni.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top