Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue |
Taarifa iliyotolewa na katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue imesema hatua hii inakuja baada ya hapo awali, Serikali kuwatumia zaidi wataalamu kutoka nchi nyingine, ambapo kwa sasa lengo ni kuona kwamba wataalamu wa nchi nyingine wanatumika pale tu ambapo wataalamu wa Kitanzania walio ndani na nje ya nchi hawajapatikana kufanya kazi husika.
Taarifa hiyo imeainisha maeneo yenye uhitaji wa wataalamu hao wa Kitanzania kuwa ni pamoja na Mfumo mzima wa utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na usambazaji wa gesi asilia na mafuta, uimarishaji matumizi salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano -TEHAMA katika kuboresha utendaji wa Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Pia taarifa hiyo imetaja eneo jingine linalohitaji wataalamu hao kuwa ni uboreshaji wa utekelezaji wa malengo ya Serikali na kupima matokeo kupitia mfumo unaokusudiwa kuhakikisha tunapata matokeo makubwa na ya haraka katika maeneo ya kipaumbele na kimkakati katika maendeleo ya Taifa.
Wataalamu watakaojitokeza na kukubaliwa kufanya kazi Serikalini katika maeneo hayo, watafanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi, lakini inayoweza kuongezwa iwapo utendaji utaridhisha. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment