Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii DK Hussein Mwinyi

Serikali imesema itahakikisha kuwa haki za msingi kwa  watu wasioona zinazingatiwa kwa ustawi wa kundi hilo maalum katika jamii.Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dakta Hussein Mwinyi ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya maandishi nundu kwa watu wasioona.
 


Waziri Mwinyi pia amesema serikali itasaidia katika ujenzi wa  kiwanda kidogo cha kutengeneza fimbo nyeupe ambazo hutumiwa na watu wasioona. Waziri huyo ameitaka jamii kuwapeleka shule watoto wote wenye matatizo ya uoni hafifu badala ya kuwaficha ili wapate fursa sawa ya kuelimika kama ilivyo kwa makundi mengine.
 

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi, mwakilishi wa wasioona Bi Sophia Shabani amesema uhaba wa vitabu vyenye maandishi ya nukta nundu, fimbo nyeupe na uchakavu wa mitambo ya kuchapia machapisho mbalimbali ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili watu wenye matatizo ya uoni. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top