Wanajeshi wa JWTZ wakibeba jeneza lenye mmoja wa askari wenzao saba
waliouawa kwa shambulio la ghafla wakiwa katika Jeshi la Ulinzi wa Amani
la Umoja wa Mataifa mjini Darfur, jumamosi iliyopita. Miili hiyo
iliwasili leo saa 10.30 jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kikosi cha Anga
cha JWTZ.
Baadhi ya viongozi wakiongozwa na Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gharib
Bilal wakishuhudia miili ya wanajeshi saba wa JWTZ waliouawa na waasi
mjini Darfur, miili hiyo ilipofikishwa leo Uwanja wa Ndeje wa Kikosi cha
anga cha JWTZ jijini Dar es Salaam.
Askari wakiingiza mwili mmoja wapo kati ya miili saba katika gari la jeshi tayari kuisafirisha.
Baadhi ya wananchi wakiwa hawaamini wanchokiona
Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi
Job Masima wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kikosi cha Anga cha JWTZ, kabla ya
miili kuwasili. Wengine kulia ni Ridhiwani Jakaya Kikwete, Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa CCM
(Bara), Mwigulu Nchemba. ambao walihudhuria mapokezi ya miili hiyo.
Makamu wa Rais, Dk. Muhammed Gharib Bilal akimsalimia Katibu Mkuu wa
CCM, Kanali Mstaafu, Abdurhaman Kinana, baada ya kuwasili kwenye
mapokezi ya miili ya wanajeshi hao. Katikati ni Waziri wa Ulinzi Shamshi
Vuai Nahodha
Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gharib Bilal akimsalimia Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi Nape Nnauyebaada ya kuwasili kwenye Mapokezi ya miili
ya askari wa JWTZ waliouawa mjini Darfur
Makamu wa Rais, Dk. Muhamed Gharib Bilal akiagana na Mkuu wa Majeshi,
Jenerali Davis Mwamunyange, baada ya mapokezi ya wanajeshi wa JWTZ
waliouawa Darfur kukamilika
Ndugu wa mmoja wa askari wa JWTZ waliopoteza maisha kwa kushambuliwa na
waasi mjini Darfur akiwa mwenye majozi wakati wa mapokezi ya askari
hao.
Msafara wa malori saba yaliyobeba miili ya askari saba wa JWTZ waliouwa
Darfur uliongozwa na polisi wakati wa kutoka Uwanja wa Ndege, Kikosi cha
Anga baada ya kupokewa leo jioni.
Picha zote na theNkoromo Blog
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment