VAN PERSIE AIPAISHA MAN UNITED
Robin van Persie
Vinara wa ligi kuu England Manchester United  wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwachapa mahasimu wao Liverpool kwa magoli 2 – 1 katika mechi ya ligi kuu England.
 Man United ambao walikuwa nyumbani Old Trafford walipata goli lao la kwanza dakika ya 19 kupitia kwa Robin van Persie aliyepata pasi kutoka kwa Patrice Evra, bao ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Dakika ya 54 beki Nemanja Vidic aliifungia goli la pili Man U baada ya pasi ya mwisho kutoka kwa Patrice Evra, Hata hivyo shangwe za goli hilo kwa mashabiki wa Red Devils hazikudumu kwani Dani Sturridge aliifungia Liverpool goli la kufutia machozi dakika ya 57.
Kwa matokeo hayo Man United imefikisha pointi 55 kileleni huku Liverpool ikibakia na pointi zake
ARSENAL YAANGUKIA PUA NYUMBANI
Adin Dzeko
Katika mechi nyingine ya "Super Weekend" nchini England ilikuwa baina ya washika bunduki wa London Arsenal dhidi ya Manchester City ambapo wenyeji Arsenal wamekubali kichapo cha magoli 2 – 0 mechi ikichezwa katika dimba la Emirates.
Arsenal ilipata pigo mapema kabisa dakika ya tisa pale beki wake alipolimwa kadi nyekundu kwa kumfanyia madhambi ndani ya penati boksi Edin Dzeko ambapo Mwamuzi aliamuru penati kupigwa. Edin Dzeko alipiga penati hiyo ambayo iligonga mwamba na kuokolewa na golikipa wa Arsenal. 
James Milner Miner akaifungia goli la kwanza Man City huku Edin Dzeko akirekebisha makosa  kwa kuifungia goli la ushindi.
Baada ya kucheza kwa kipindi kirefu ikiwa pungufu dakika ya 74 mzimu wa kadi nyekundu ukawaangukia  Man City ambapo nahodha na beki wake Vincent Kompany alioneshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya Jack Wilshere.
Kwa matokeo hayo Man City imefikisha pointi 48 ikiendelea kujikita katika nafasi ya pili.

 NENE KUKIPIGA UARABUNI
Nene
Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil NENE anataraji kujiunga na klabu ya Al Gharafa ya Qatar akitokea Paris St Germain ya Ufaransa.
NENE(31) aliifungia PSG magoli 21 msimu uliopita, anataraji kusaini mkataba wa miezi 18 ambao utampatia kiasi cha Euro milioni 16.
Mchezaji huyo ameichezea PSG mechi 79 na kuifungia magoli 36 lakini msimu huu amecheza mechi tisa tu.

Matokeo mengine ya ligi kuu England.


Queens Park Rangers
0-0
Tottenham







Aston Villa
0-1
Southampton







Everton
0-0
Swansea







Reading
3-2
West Bromwich Albion







Norwich
0-0
Newcastle United







Stoke
0-4
Chelsea







Fulham
1-1
Wigan





TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top