THOMAS
MASHALI ATETEA UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI.
Bondia Mtanzania Thomas Mashali
ameweza kuutetea mkanda wake wa ubingwa wa Afrika Mashariki na kati baada ya
kumtwanga Mkenya Benard Mackoliech katika pambano kali na la kusisimua
lililopigwa katika ukumbi wa Friends Corner Manzese jumamosi usiku.
Pambano lilikuwa kali lakini kukosekana umakini (timing mbovu) kwa Benard zilimfanya alambe sakafu karibu mara
tatu katika raundi ya nne,tano na sita ambapo alisalimu amri baada ya
kuhesabiwa na Mwamuzi Mark Hatia.
Bondia Mtanzania
Thomas Mashali kushoto akiwa amemlambisha sakafu Mkenya Bernad Mackoliech na kwenda chini akimsubiri
ainuke wakati wa mchezo wao wa kugombania ubingwa wa Afrika Mashariki
uliofanyika katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam na Mashali
kuibuka na ushindi kwa KNOCK OUT katika raundi ya sita.
Kama vile sako
la nyani ngedere haponi hapa mabondia Bernad Mackoliech wa kenya na Mtanzania
Thomas Mashali wakioneshana ufundi wa kutupiana makonde wakati wa mchezo wao wa
ubingwa wa Afrika Mashariki Mashali alishinda kwa K,O raundi ya sita.
Kamanda wa
mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Charles Kenyela akifuatilia kwa makini Pambano la
ngumi baina ya bondia Mtanzania Thomas Mashali na Mkenya Benard Mackoliech
lililofanyika katika ukumbi wa Friends
corner Manzese jijini Dar es Salaam.
Charles Kenyela
akimvisha mkanda wa ubingwa wa Afrika Mashariki na kati Thomas Mashali (Simba
Asiyefugika) baada ya kumbwaga mpinzani wake benard Mackoliech.
Baadhi ya Mashabiki waliojitokeza wakishangilia mara baada ya
ushindi wa bondia Mtanzania Thomas Mashali dhidi ya Mkenya Benard Mackoliech
jana usiku.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment