![]() |
Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura |
Release No. 03
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Januari 14, 2013
WAGOMBEA TFF
KUPATA FOMU KWENYE TOVUTI
Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawaarifu wadau
wote kuwa fomu za maombi ya uongozi wa TFF na Tanzania Premier League Board
(TPL Board) zinapatikana pia kwenye tovuti ya TFF.
Wote
wanaopenda kugombea uongozi katika vyombo hivyo wanaarifiwa kuwa wanaweza
kupata fomu hizo kwenye tovuti ya TFF (www.tff.or.tz) na wanatakiwa
kulipia fomu hizo katika akaunti ya TFF namba 01J1019956700 iliyoko CRDB tawi
la Holland House.
Fomu
zikiambatanishwa na risiti ya malipo (receipt) au malipo ya benki (deposit
slip) zirejeshwe kwa Katibu Mkuu wa TFF kwa mkono au kwa barua pepe (email)
ambayo ni tfftz@yahoo.com kabla ya saa
10 kamili alasiri ya Januari 18 mwaka huu.
Kwa
wagombea wanaorejesha fomu kwa mkono kuna fomu ya orodha (register) ambayo
wanatakiwa kusaini wakati wanakabidhi.
Kamati ya Uchaguzi
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
PONGEZI KWA
UONGOZI MPYA RUREFA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika
Januari 10 mwaka huu.
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa RUREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo
huo mkoani Rukwa.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya RUREFA chini ya
uenyekiti wa Blassy Kiondo aliyeibuka mshindi katika uchaguzi huo uliofanyika
mjini Sumbawanga.
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli
za mpira wa miguu mkoani Rukwa kwa kuzingatia katiba ya RUREFA pamoja na vyombo
vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za
Wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Blassy Kiondo (Mwenyekiti), Gregory Seko
(Katibu), John Maholani (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Ayoub Nyaulingo
(Mwakilishi wa Klabu TFF) na Gloria Ndawa (Mweka Hazina). Nafasi nyingine
zitajazwa katika uchaguzi mdogo.
HONGERA KWA
AZAM KUTWAA KOMBE LA MAPINDUZI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi wa klabu ya Azam
kwa timu yao kufanikiwa kutwaa Kombe la Mapinduzi mwaka huu.
Kwa
Azam kufanikiwa kutetea ubingwa huo inaonesha jinsi klabu hiyo ilivyojipanga
kabla ya kuingia katika mashindano hayo ambapo ilicheza fainali dhidi ya Tusker
FC ya Kenya.
Pia
ushindi huo utakuwa changamoto kwa timu nyingine za Tanzania Bara zitakazopata
fursa ya kushiriki michuano hiyo ya Kombe la Mapinduzi mwakani. Michuano hiyo
iko kwenye Kalenda ya Matukio ya TFF.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment