Mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii wa LAPF kwa serikali za mitaa umewataka wanachama kuwekeza mafao yao kwenye mfuko huo  ikiwa ni njia salama ya kulipwa mafao bora kwenye mfuko huo.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja wa mfuko wa LAPF FORTUNE MAGAMBO  amesema kuwa mfuko huo unaendelea kuboresha huduma yao kwa wanachama  pamoja na kuimarisha utendaji bora wa kazi hapa nchini.

Naye  meneja masoko  ANDREW KUYEYEWA amesema kuwa mfuko huo umekuwa ukisaidia jamii kwa kutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama,  kusaidia walemavu wa ngozi  na watoto yatima hapa nchini

 Meneja  huyo amezungumzia changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na watu zaidi ya million 18 hawafaidiki na mfuko huo na wengine kutofikiwa na huduma hiyo.

Aidha mfuko huo umekuwa ukiongoza kwa kupata tuzo kwa muda wa miaka 4 mfululizo ikiwa ni moja ya kutoa na kufunga hesabu zake kwa wakati sahihi.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top