Serikali imetakiwa kushughulikia kikamilifu madai ya fidia kwa wakazi wa Mbagala walioathirika na mabomu Aprili mwaka 2009.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya waathirika hao wamesema hawana imani  na zoezi la uthamini ambalo limerejewa mara tano mpaka sasa huku likiacha malalamiko kwa zaidi ya wakazi 1700.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Steven  Gimongi amesema ni muda mrefu umepita tangu tukio hilo litokee na gharama za vifaa vya ujenzi zinazidi kupanda hivyo kuchangia uwezekano wa nyumba zao kutokarabatiwa
  
Mwenyekiti huyo amesema wameshangazwa na ukimya wa serikali kushindwa kulipa fidia huku wakishuhudia wenzao wa Gongola Mboto wakiwa wameshatimiziwa masuala yao baada
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top