Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini Sumatra imeyafungia mabasi 65 ya abiria kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kupandisha nauli. Afisa wa mamlaka hiyo kanda ya mashariki Konradi Shio amesema hatua hiyo ya Sumatra imekuja baada ya mabasi hayo kubainika kupandisha nauli kiholela pamoja na matumizi mabaya ya leseni. Amesema adhabu hiyo ya  siku 15 inaanza kesho na inahusisha baadhi ya mabasi yanayofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Mtwara,Dar es salaam na Morogoro na Dar es salaam na Mwanza. Afisa huyo amewaonya wamiliki wa mabasi kuepuka tamaa ya fedha huku akiwataka abiria kununua tiketi katika ofisi rasmi za mabasi hayo
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

1 comments:

Unknown said... December 14, 2012 at 9:23 PM
This comment has been removed by the author.
 
Top