Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litatuma ofisa wake nchini mwezi ujao kwa ajili ya kufanya ukaguzi kwenye klabu za Ligi Kuu ya Tanzania.

Kwa mujibu wa CAF, ofisa huyo atakuwa nchini kuanzia Januari 7 mwakani ambapo atafanya ukaguzi huo hadi Januari 14 mwakani. Mbali ya ukaguzi katika klabu, pia ofisa huyo atakagua viwanja vitakavyotumika katika mashindano yake na hoteli ambazo timu kutoka nje zitakuwa zinafikia kabla ya mechi.Simba inaiwakilisha Tanzania katika ligi ya mabingwa barani Afrika wakati Azam itashiriki katika michuano ya Shirikisho maarufu kwa hapa nyumbani kama kombe la CAF


CAF kabla ya kutoa leseni kwa inafanya uhakiki kwa timu ambazo zitakuwa zimekidhi vigezo vilivyowekwa. Ili klabu ishiriki mashindano ya CAF ni lazima iwe na leseni hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top