Lucas Nkungu katibu mkuu wa chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,
Sara Ramadhani Mratibu wa Mashindano ya riadha maalum kuukaribisha mwaka mpya
Mashindano ya riadha maalum kuukaribisha mwaka mpya yanataraji kushika kasi hapo jumatatu usiku ukiwa ni usiku wa mkesha wa mwaka mpya 2013 kwa washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya kuchuana kusaka ushindi.
Mratibu wa mashindano hayo Mama Sara Ramadhani amesema maandalizi yote yamekamilika  huku akiwataka wanariadha wote kufika uwanja wa Taifa majira ya saa 12 jioni tayari kwa safari kuelekea Police Oficers Mess.
Mratibu huyo amesema  zawadi za mwaka huu zimeboreshwa zaidi hasa baada ya kupata udhamini kutoka kwa udhamini kutoka kwa kampuni ya Mohamed Enterpises.
Naye Katibu mkuu wa chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam, Lucas Nkungu amesema mashindano hayo yana Baraka zote na kila mwaka yanatoa fursa kwa vijana kuonesha vipaji vyao na kuwataka wakazi wa jiji  na mikoa jirani kujitokeza  kushuhudia umahiri wa  wakimbiza upepo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top