Imethibitika kwamba technolojia ya mawasiliano hivi sasa imekua kwa kasi ya ajabu sana, kiasi cha kufikia kuwa kumbe siyo lazima tutegemea camera za waandishi wa habari kuchukua matukio.

Ni kwamba chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kwenye mkutano wake wa mwisho licha ya kutumia SATELLITE kurekodi mikutano yake, imethibitika kuwa chama hicho kilitumia mtambo maalum wa mawasiliano kurekodi mkutano wake wa mwisho katika uwanja wa soweto Arusha. 

Mtambo huo ambao unauwezo wa kurekodi matukio kwa masaa 72 mfululizo bila kuhitaji chaji, ulifungwa sehemu maalum ili kuweza kunasa matukio yaliyokuwa yanaendelea kwenye mkutano.

 
Mtambo huo ulisaidia kunasa tukio la mlipuko wa bomu na matumizi ya risasi kwenye mkutano kuwapiga raia, ambapo ulionyesha askari polisi aliyesimama pembeni ya nguzo ya umeme karibu na mfereji ulio mkabala na round about iliyo karibu na soweto garden akiwapiga risasi watu waliokuwa wanamkimbiza mtu aliyevaa suruali ya jeans aliyekimbia nakuingia kwenye gari ya polisi na kuondoka kwa kasi kwenye eneo la tukio.

 Mtambo pia uliweza kuonyesha gari ya blue landcruiser iliyoweza kui escort gari ambayo amepanda yule mtu aliyekuwa anakimbizwa.

Ule mtambo ambao una uwezo wa kurekodi matukio kwa around 360 degree angle uliweza kuonyesha tukio la watu wanaosadikiwa kuwa maaskari kufika kwenye eneo la tukio hasa kwenye gari la matangazo la chadema majira ya usiku, na kuweza kuzurura pale bila kuonyesha kwa kina walichokuwa wanakifanya pale.

video inaonyesha ule mtambo ulizima wenyewe saa moja na madakika asubuhi ya siku ya pili.

Kwa ujumla mtambo una taarifa nyeti za kuweza kusaidia kwa ushahidi wa tukio hili ambalo limegharimu maisha wa watu wasiokuwa na hatia. 

Muda utakapofika nadhani kwa idhini ya mwenyekiti wa chama kila kitu kitawekwa wazi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

4 comments:

Thabit said... June 21, 2013 at 11:55 AM

Kama hii habari ni kweli wamedhalilika, na hasira za wananchi zitawashukia. Tuko pamoja wanamapinduzi wa kweli.

Anonymous said... June 21, 2013 at 2:08 PM

Watatokaje hao waliohusika na kadhia hiyo? Itakuwa aibu kweli kweli. Na je waliosema kwamba wananchi waliwashambulia polisi na hivyo polisi walijihami kwa kufyatua risasi itakuwaje kwao? Haialishi kwamba hawatachukuliwa hatua yoyote lakini ninajua na kuamini kwamba HAKI itajitetea ole wao walishiriki.

Anonymous said... July 16, 2013 at 9:37 AM

mimi sina la kusema la mhimu kabisa mimi km mwanaharakati ambae nahitaji ukomboz ifikapo hawa mbwaa wanahitaji kupewa live wapewe na ole waooo tutawanyongaa 2015 naishia hapa mana ninahasira kubwaa

 
Top