JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA LINAPENDA KUTOA WITO KWA WANANCHI WOTE KUSHEHEREKEA
SIKUKUU YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA
ITAKAYOADHIMISHWA USIKU WA TAREHE 3I/12/2012 KUAMKIA TAREHE 1/12/2013
KWA AMANI NA UTULIVU, PASIPO VITENDO AMA VIASHIRIA VYOVYOTE VYA UVUNJIFU WA
AMANI NA SHERIA ZA NCHI.
IKUMBUKWE KUWA, WANANCHI WENGI HUTUMIA MUDA HUO KWENDA KUMSHUKURU MUNGU
KATIKA NYUMBA ZA IBADA KWA MAMBO MBALIMBALI AMBAYO MWENYEZI MUNGU AMEWATENDEA
KWA KIPINDI CHOTE CHA MWAKA.
PAMOJA NA HILO KUTAKUWA NA MUENDELEZO WA SHEREHE HIZO KWENYE MAENEO
MBALIMBALI YA STAREHE. HATA HIVYO, UZOEFU UNAONYESHA KUWA BAADHI YA WATU
HUTUMIA KIPINDI HICHO CHA SIKUKUU KUFANYA MATUKIO YA UHALIFU.
JESHI LA POLISI LINAPENDA KUWAONDOA
HOFU WANANCHI WOTE KUWA, LIMEJIPANGA KIKAMILIFU. KUKABILIANA NA YEYOTE YULE MWENYE NIA
YA KUTENDA KITENDO CHOCHOTE CHA UVUNJIFU WA AMANI. ULINZI UTAIMARISHWA KWENYE MAENEO YOTE YA IBADA, SEHEMU ZA STAREHE NA
MAENEO MENGINE YOTE AMBAYO YATAKUWA NA MIKUSANYIKO MIKUBWA YA WATU.
AIDHA, TUNAPENDA KUWATAHADHARISHA KWA WALE WOTE AMBAO
WATAKUWA WAKITUMIA BARABARA, KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA
BARABARANI NA HASA KWA MADEREVA KUEPUKA KWENDA MWENDO KASI NA KUTUMIA VILEVI. TUTAKUWA
WAKALI NA TUTAPIMA MADEREVA KILEVI.
KWA WALE WENYE KUMBI ZA STAREHE, WAZINGATIE SHERIA NA UHALALI
WA MATUMIZI YA KUMBI ZAO KATIKA UINGIZAJI WA WATU KULINGANA NA UWEZO WA KUMBI
HIZO, BADALA YA KUENDEKEZA TAMAA YA FEDHA KWA KUJAZA WATU KUPITA KIASI.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment