Kituo kimoja cha televisheini
nchini Australia kilichoonyesha kanda ya video ya mwanariadha Oscar
Pistorius akisimulia kilichotokea hadi akamuua mpenzi wake, imejitetea
kwa kupeperusha kanda hiyo.
Channel 7 imesema kuwa iliipata kanda hiyo kwa njia halali.
Kanda hiyo ilipeperushwa tu katika
stesheni hiyo Jumapili na kinamuonyesha Pistorius akipiga mayowe na
kukimbia kwa miguu yake bandia huku akishika bunduki.
Utetezi unatafakari kuhusu kumaliza kutoa ushahidi.
Kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha mlemavu
Oscar Pistorius imeanza kusikilizwa tena leo, huku picha za video
zinazomuonyesha mwanariadha huyo akisimulia alivyomuua mpenzi wake Reeva
Steenkamp zikiwa zimetolewa.
Wakili wa Pistorius amevilaumu vyombo vya habari
vya Australia kwa kurusha picha hizo za video kwa madai kuwa
zilipatikana kinyume cha sheria.
Mwandishi wa BBC nchini Afrika kusini anasema
huenda ushahidi ulioonyeshwa kwenye picha hizo ukatumika katika
mashitaka hayo ya Pistorius.
Picha hizo zimeonyeshwa jana katika runinga moja
nchini Austarilia, msemaji wa Pistorius amesema kuwa picha hizo
zilichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kisayansi japo kuwa ilikuwa
katika mfumo ambao ni kinyume cha sheria.
"Kwa upande wa familia kurushwa kwa picha hizo
ni kama kuingilia uhuru binafsi” anasema msemaji huyo. Hata hivyo picha
hizo hazijawahi onyeshwa nchini Afrika Kusini ambako ndiko kesi hiyo
imekuwa ikiendeshwa.
Mwandishi wa BBC Andrew Harding aliyepo Afrika
Kusini anasema haifahamiki mara moja kwanini picha hizo hazikutumika
kama kielezo katika kesi ya Pistorius.
Pistorius mwenyewe ameendelea kusisitiza kuwa
alimuua mpenzi wake kwa bahati mbaya akidhani kuwa walikuwa wamevamiwa
na majambazi.
Mwanariadha huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Steenkamp kwa takribani miaka mitatu kabla ya mauaji hayo.
BBC
0 comments:
Post a Comment