Wandishi hao walifungwa jela kwa kati ya miaka 7 na kumi.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ameliambia gazeti moja nchini humo kuwa anajutia uamuzi wa mahakama kuwafunga jela wandishi wa tatu wa shirika la habari la Al Jazeera. 

Bwana Al Sisi amesema kuwa waandishi hao watatu walipaswa kuamrishwa kurejea makwao badala ya kuhukumiwa kifungo jela.
Kwenye mkutano na wandishi habari rais Al-sisi alisema kuwa kuhukumiwa kwa waandishi hao kumeonyesha picha mbaya kuhusu Misri.

Waandishi hao walihukumiwa kifungo cha kati ya miaka 7- 10 gerezani kwa kueneza habari za uongo na kulisaidia kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood.

Muda mfupi baada ya hukumu hiyo rais Al sisi alisema kuwa hawezi kuingilia shughuli za mahakama.
Al Sisi amesema hukumu hizo zilitoa picha mbaya kuhusu Misri
Lakini matamshi yake ya hivi punde yametoa matumaini kwa familia za mwaandishi wa habari raia wa Australia Peter Greste na mwenzake mwenye asili ya Canada na misri Mohammed Fahmy
Nduguye Peter Greste Andrew amesema kuwa matamshi hayo yamempa matumaini.

Naye nduguye Mohammed Fahmt amesema kuwa hii ni ishara kwamba jambo fulani ni lazima lifanywe.

Lakini familia ya mwandishi mwingine wa tatu aliye kizuizini Baher Mohammed ilipuunza matamshi hayo na kuyataja kuwa ya kuchekesha.

Waandishi hao wote watatu wanajipanga kukata rufaa.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top