
Watu walioathirika na vita mjini Bangui
Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba
Panza, ameapa kuwa atapambana na wapiganaji wa Kikristu ambao walihusika
na mashambulio ya hivi karibuni dhidi ya Waislamu katika mji mkuu wa
nchi hiyo Bangui.
Rais Samba-Panza amesema waasi hao, wanaojulikana kama, 'wanaopinga-balaka,' wamepoteza mwelekeo na hawana dhamira yoyote.
Amesema wapiganaji hao ambao walikuwa watetezi wa jamii, wamegeuka na kuwa wauaji na waporaji.
Maelfu ya Waislamu wameukimbia mji huo na kukimbilia nchi jirani ya Cameroon.
Hata hivyo ushahidi wa mauaji ya halaiki yaliyotekelezwa na wapiganaji wa Seleka unaendelea kutolewa.
Misikiti yabomolewa
Mwandishi wa BBC, mjini Bangui, Kassim Kayira,
anasema kuwa, Waislamu wengi wamepiga kambi katika msikiti mkubwa zaidi
nchini humo, baada ya misikiti mingine kuharibiwa, huku Wakristu nao
wakipiga kambi karibu na uwanja mkuu wa Ndege.

Watu wakiwa kambini mjini Bangui
Aidha amesema hali katika kambi hiyo ni ya
kusikitisha huku wakimbizi hao wa ndani wakihitaji misaada ya dharura
kama vile vyakula na dawa.
Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty international limesema kinachotokea CAR ni kumalizwa kwa jamii.
Ripoti hiyo imetolewa wakati maelfu ya Waislamu wanaendelea kuukimbia mji mkuu Bangui wakielekea nchi jirani.
Wakati huo huo Shirika la mpango wa chakula
duniani WFP linasema ndege ya kwanza iliyosheheni misaada imewasili
katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya kati Bangui.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment