
Wahifadhi wakuu wa mazingira kutoka kote duniani
wanakutana mjini London Uingereza kubuni mikakati ya kukomesha uwindanji
haramu wa wanyamapori walio katika hatari ya kuangamia.
Moja ya malengo ya wadau hao ni kumulika
changamoto wanazokabiliwa nazo wanyama pori kama Vifaru na Ndovu ambao
huenda wakaangamia katika kipindi cha miaka 15 ikiwa uwandaji haramu
hautakomeshwa.
Wanaharakati wanasema kuwa soko la pembe za wanyama hao linachochewa na biashara nchini China.
Mkuu wa shirika la kulinda wanyamapori nchini
Kenya, Paula Kahumbu ameambia BBC kuwa madhumuni ya kongamano hilo ni
kuona kuwa China inaharamisha biashara ya pembe za Ndovu na vifaru.
Kahumbu anasema kuwa biashara haramu ya
wanyamapori zisingekuwa zinafanyika ikiwa serikali za Kenya, Uganda na
Tanzania zingechukua hatua kali.
Alisisitiza kuwa ufisadi unaruhusu watu
kusafirisha makonteina makubwa makubwa yenye pembe za Ndovu na Vifaru
kutoka Afrika. Pia ametoa wito kwa China kuharamisha biashara ya Pembe
za Ndovu.
Wajumbe kutoka nchi 46 na mashirika 11 ya
kimataifa, watahudhuria kongamano hilo, wakiwemo marais kadhaa wa nchi
za Afrika ambazo ziomejitolea kupambana na uwindaji haramu wa Ndovu na
Vifaru.
Moja ya nchi ambazo zinatoa adhabu kali kwa
watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na biashara haramu ya pembe za
Ndovu au Vifaru ni Kenya.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment