
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amewafuta kazi mawaziri wanne akiwemo waziri wa usafiri wa angani.
Mwaka jana Stella Oduah alihusishwa na kashfa ya kutumia dola milioni moja unusu kununua magari mawili.
Mabadiliko haya ya serikali yanakuja
mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais na wakati ambapo wanasiasa
kadhaa kutoka chama tawala wamehamia upinzani.
Hatua ya Goodluck Jonathan kuwafuta kazi mawaziri sio jambo la kushangaza.
Hivi karibuni Rais Goodluck alifanya mageuzi
makubwa ambayo yanaonekana kulenga kuboresha nafasi yake ya ushindi
katika uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Lakini kilichowashangaza wengi ni kufutwa kazi kwa Stella Oduah mabaye alikuwa mshirika wa karibu wa Rais Goodluck na mtu muhimu katika kuchangisha pesa za uchaguzi mkuu uliopita.
Hata hivyo mwaka jana Stella Oduah alihusishwa
na madai ya ufisadi wakati ambapo wanigeria walikuja kujua kuwa wizara
yake ilitumia zaidi ya dola milioni moja kununua magari mawili ya BMW
yanayoweza kuhimili risasi.
Alikanusha kuhusika na ufisadi.
Wengine waliopoteza kazi zao ni Waziri wa maswala ya polisi, waziri wa maswala ya Niger Delta na waziri wa fedha.
Rasmi walijiuzulu lakini nchini Nigeria hii
inaonekana kama sio hatua kali kwa kosa la ufisadi. Ingawa bado
hajatangaza nia yake ya kuwania urais, tetesi zinaarifu kuwa huenda
akawania.
Lakini huenda akakabiliwa na ushindani mkali
kutoka kwa chama cha upinzani APC, ambao umefaidika pakubwa kutokana na
wanasiasa mashuhuri kukikahama chama tawala PDP.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment