Kamanda Kova
 Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limeunda jopo la wapelelezi kuchunguza tuhuma zinazowakabili askari wanaodaiwa kugawana fedha taslimu shilingi milioni 150 zilizonusurika kuporwa katika tukio la ujambazi Kariakoo
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amesema jopo hilo limeundwa kufuatia taarifa zilizotolewa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa askari hao waliochukua fedha hizo walikwenda kugawana katika eneo la Jangwani.
Amesema jopo hilo litaongozwa na mkuu wa upelelezi kanda maalum Ahmed Msangi na moja ya majukumu ni kuhakikisha kuwa ukweli kuhusu tuhuma hizo unapatikana katika muda mfupi inavyowezekana

Fedha hizo zilikuwa zikipelekwa benki na wafanyabiashara wenye asili ya Somalia kabla ya kuvamiwa na majambazi maeneo ya mtaa wa Mahiwa na Livingstone Kariakoo kabla ya kuokolewa na askari hao ambapo mtu mmoja alipoteza maisha



  

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top