Taarifa
iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya MCC
katika kikao chake kilichofanyika tarehe 19 Desemba, 2012 imebainisha majina ya
nchi tano zenye sifa ya kupatiwa msaada huo wa fedha kutoka MCC na kuzitaja nchi hizo kuwa ni
Tanzania, Liberia, Niger, Sierra Leone na Morocco.
Hivi sasa nchi
hizo zinatakiwa kuandaa mapendekezo ya mipango yao ya maendeleo kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali, kwa ajili ya kupatiwa msaada wa fedha kwa
awamu nyingine.
Kwa mujibu wa
Afisa Mtendaji wa MCC, Bwana Daniel
W. Yohannes, Tanzania na Morocco zimeendelea kufanya vizuri katika matumizi ya
fedha za MCC zilizotolewa katika
Awamu ya Kwanza na akabainisha kuwa nchi hizo zimekuwa washirika wazuri katika suala
zima la utekelezaji. Sifa za kupatiwa
fedha kutoka MCC kwa awamu nyingine
zinategemea utekelezaji mzuri wa mipango ya maendeleo inayojielekeza zaidi katika
shughuli za kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
Katika Awamu
ya Kwanza, Tanzania ilipatiwa msaada wa fedha kutoka MCC wa jumla ya Dola za Marekani 698.1 milioni ambazo zimetumika
katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kupunguza
umaskini hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment