Watu nchini Israel leo wanaanza kipindi kifupi cha
maombolezi kufuatia kifo cha waziri mkuu wa zamani Ariel Sharon
aliyefariki akiwa na umri wa miaka 85 baada ya miaka 8 ya kuwa hali
mahututi.
Wananchi watatoa heshima zao za mwisho kwa mwili wake Jumapili kabla ya kuzikwa Jumatatu.
Viongozi wa dunia wametoa rambi
rambi zao kwa Sharon, mtu aliyepigana katika vitaa vikuu vinne kabla ya
kuingia katika ulingo wa siasa.
Lakini aliwaacha wapalestina wengi waliomuona kama adui wao wakiwa na hamaki.
Mkuu wa kituo cha afya cha Sheba mjini Tel Aviv
alithibitisha kifo cha Sharon, Jumamosi mchana siku ya Sabato kwa
wayahudi, zaidi ya wiki moja baada ya taarifa kutolewa kuhusu afya yake
kuzorota.
Mmoja wa wanawe Sharon,Sharon, Gilad Sharon, alisema kuwa babake amekwenda wakati alipoamua mwenyewe kwenda.
Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle
Obama, wamesema Sharon, alikuwa kiongozi aliyejitolea kuwahudumia watu
wa Israel.
Rais Shimon Peres, mwandani mkuu wa Sharon japo
alikuwa hasimu wake wa kisiasa aliyejiunga na serikali ya Muungano na
Sharon mwaka 2001, alisema Sharon alikuwa mtu mwema aliyepigania watu
wake na kuwapenda na kuwa watu pia walimpenda.
Wadhifa wa Sharon kama waziri mkuu ulifika
kikomo baada ya kupatwa na kiharusi na kisha kuwa katika hali mahututi
kwa miaka minane tangu mwaka 2006.
Wakati huu wote alikuwa anatumia mashine kupumua na mirija kulishwa chakula.
Kabla ya hali ya Sharon kuzorota aliongoza jeshi
la Israel kuondoka katika ukanda wa Gaza ili kupunguza taharuki kati ya
Israel na Palestina.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment