Mkuu wa mkoa Iringa Dr Christine  Ishengoma akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano ofisini kwake tar,10/01/2014 wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi  kwa kipindi cha miezi sita Julai-Desemba 2013. 

 Pichani waandishi wa habari mkoa wa Iringa na maafisa ofisi ya Mkoa wakimsikiliza Mkuu wa Mkuu  Dr Christine .G.Ishengoma wakati akito taarifa ya kazi.

 Afisa kilimo Mkoa wa Iringa Paulo Msangi  akifafanua jambo kuhusu Idara yake wakati wa maswali na majibu baada ya taarifa ya mkuu wa mkoa Iringa.

Taarifa hiyo ilio jumuisha shughuli zifanyikazo katika mkoa wa Iringa kwa ujumla kama Sekta ya kilimo na uzalishaji mali.

kwamapinduzi ya kilimo kumekuwa na ongezeko la matumizi ya zana za kilimo Matrekta makubwa,madogo na zana zakukokotwa na wanyama kazi kwa asilimia 0.23 kwa mwaka 2013-2014.


 kulikopelekea ongezeko la uzalishaji mazao kwamfano  mahindi kutoka tani 549,363.5 mpaka 676,936.


Hivyo kumeongeza uzalishaji mazao yote kwajumla kwakuwa kulikuwepo na upatikanaji wa pembejeo na matumizi yake kwa wakulima.



Kwa upande wa umwagiliaji jumla ya hekta 2,080 za mpunga zinalimwa katika skimu za umwagiliaji nakufanya kuwe na ongezeko la asilimia 46% taka 31% kuliko pelekea kuvuna tani 58,370.

Mapinduzi ya mifugo na mafunzo kwa wafugaji elimu imetolewa katika vijiji 34 vya mkoa wa Iringa nyanda za malisho na Afya ya mifugo pamoja na Mradi wa kopa Ng'ombe lipa Ng'ombe. na vikundi 47 vilipata Elimu.

Pamoja na hayo taarifa hiyo imejumuisha Sekta za Utalii,Viwanda,Biashara na masoko pamoja na kuendelea kuhamasisha Jamii kutumia bidhaa zinazo zalishwa ndani na kuwajengea uwezo wa ujasiliamali.

Sekta ya miundo mbinu kumekuwepo na upimaji wa mipaka ya vijiji,Mashamba,Viwanja na utoaji wa Hati miliki
Kuandaa michoro 8 ya Mipangomiji na kupima viwanja2160 katika halmashauri Wilaya za Iringa Manispaa na Mufindi.

Matengenezo ya barabara maeneo korofi jumla ya km.218.7 katika Halmashauri za Iringa ,manispaa na kilolo zinahitaji matengenezo ya kawaida zipo katika hatua ya kuwapata wakandarasi na Km.22 katika wilaya ya Mufindi zimetengenezwa.

Pia kuna matengenezo maalumu jumla ya km.83.16 katika halmashauri zote zinafanyiwa matengezo ya muda maalumu na zipo katika hatua mbalimbali za Ujenzi.

Sekta ya uwezeshaji wananchi kiuchumi jumla ya saccos 2 zimeundwa na kufanya jumla ya saccos 270 pia mikopo yenye thamani ya Tsh.11,525,000/= kwenye halmashauri ya Wilaya ya Iringa

 Uboreshaji wa elimu ya msingi na Sekondari, Afya na huduma ya maji, pia kuwaongezea uwezo wananchi kukabiliana na majanga wananchi wanaendelea kupewa elimu katika halmashauri zote.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top