Dk. Wilbrod Slaa akiwasili katika uwanja wa Shule ya Msingi Jojo

Dk. Wilbrod Slaa akiteta jambo na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Mbeya.

Mbunge wa Mbeya Mjini, ndugu Joseph mbilinyi akiteta jambo na mgombea wa udiwani kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), ndugu Elisha Mwandele.

Dk. Wilbrod Slaa akihutubia umati wa wananchi jana katika uwanja wa Shule ya msingi Jojo kata ya Santilya-Wilaya ya Mbeya Vijijini katika kampeni za kumnadi mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).
Badhi ya wananchi wakimsikiliza Dk. Wilbrod Slaa
 Mgombea wa Udiwani kata ya Santilya, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndugu Elisha Mwandele akijinadi huku Dk. Wlibtrod Slaa akimfuatilia kwa karibu.
Dk. Wilbrod Slaa akielekea katika ndege tayari kuondoka huku mvua ikinyesha.
Walinzi wa Chama (Red Brigade) wakilinda eneo ambalo ndege imeegeshwa wakati Dk. Slaa na wenzake wakiwa ndani.
Dk. Slaa na wenzake wakiwa katika helikopta wakisubiri hali ya hewa itengamae baada ya kuona eneo lote likiwa na ukungu mzito uliochagizwa na mvua ambapo iliwachukua muda wa saa moja na dakika kumi katika ndege hii.
Helikopta ikiwa bila watu baada ya Dk. Slaa na wenzake kulazimika kushuka na kuelekea katika kijiji cha Ilembo kata ya Ilembo Mbeya Vijijini yaliko makao makuu ya Tarafa ya Isangati.

Dk. Slaa akishuka katika gari (T885 BLQ) iliyompeleka katika kijiji cha Ilembo kwa mapumziko na mbele yaje (Mwenye nguo nyeusi) ni mbunge wa Mbeya mjini ndugu Joseph Mbilinyi wakielekea iliko helikopta. .
DK. Slaa akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wakimsubiri baada ya kurejea katika Uwanja wa Shule ya Msingi Jojo.
Dk. Slaa akipanda kwenye helikopta tayari kwa safari na nyuma yake ni Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu).
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akipanda kwenye helikopta tayari kwa safari pia.
Hatimaye ikawa, hali ya hewa ikaruhusu ndege kuruka kisha ikaruka kuelekea katika mji wa Vwawa Wilaya ya Mbozi alikokuwa akisubiriwa na wananchi ili awahutubie. Ilikuwa ni majira ya saa nane za mchana.

Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa jana alilazimika kusubiri yapite masaa matatu kuanzia saa 5.02 asubuhi ili aondoke katika kijiji cha shule ya msingi Jojo kilichopo katika Kata ya Santilya Wilaya ya Mbeya Vijijini kutokana na eneo hilo kufunikwa na ukungu mzito ulioambatana na mvua kiasi cha kuifanya ndege ishindwe kuruka.

 Tukio hilo lilitokea jana wakati Dk. Slaa akiwa katika zoezi la kumnadi mgombea wa CHADEMA katika kata ya Santilya ambaye anachuana na mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ndugu Anthon Mboma. 

Wananchi waliokuwepo katika uwanja huo waliendelea kumsikiliza Dk. Slaa wakati akihutubia wakati mvua ikinyesha huku wengine wakitania kuwa inawezekana wazee wamekasirikia kitendo cha Dk. Slaa kutaka kuwahutubia asubuhi wananchi wachache wakati wananchi wengi wakiwa mashambani.

Msafara wa Dk. Slaa uliingia katika helikopta saa 5.02 asubuhi tayari kwa safari ya kuelekea Wilaya ya Mbozi baada ya kuhutubia wananchi lakini ukalazimika kushuka katika helikopta hiyo yapata saa 6.20 mchana baada ya hali ya hewa kuwa ya ukungu mzito na mvua zilizokuwa zikinyesha na kukatika kila mara. 

 Awali helikopita hiyo iliyombeba Dk. Slaa ililazimika kuchelewa kutua kutokana na eneo kubwa la kata ya Santilya kuwa na Ukungu ambao hata hivyo ulipungua na kuruhusu helikopta hiyo kutua muda wa saa 4.24 asubuhi.


Ilipofika saa saba mchana watu waliongezeka zaidi ingawa haikuwezekana kwa Dk. Slaa kuzungumza nao tena kwa vile alikuwa ameshamaliza hotuba yake na alipaswa kuwa katika mji wa Vwawa Mbozi.

Na azimioletublog


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top