Na Willy Sumia, Katavi
HALMASHAURI ya wilaya ya Mlele mkoani Katavi  imepitisha bajeti ya shilingi Bil 25 kwa ajili ya simu wa bajeti wa 2014/15.

Akiwasilisha bajeti hiyo mbele ya baraza la madiwani la Halmashauri hiyo mjini Inyonga mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Godwin Bene alisema kwa kuzingatia vigezo na ukomo wa bajeti vya mwaka 2014/15 halmashauri yake imepanga kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi 25,809,615,130 kutoka katika vyanzo mbali mbali vya mapato

Alisema katika makusanyo hayo kiasi cha shilingi 8,676,617,430 kitatumika kulipa watumishi mishahara ambapo mapato kutokana na vyanzo vya ndani ni shilingi 1,628,920,279 na ruzuku ya serikali ni shilingi 13,870,920,279 ambapo vyanzo vingine vya mapato vitaiingizia halmashauri yake kiasi cha shilingi 98,288,000

Bene alisema katika kuhakikisha halmashauri yake inatimiza wajibu wake fedha za miradi iliyotengwa miradi ya maendeleo ya elimu katika elimu ya msingi itatumia kiasi cha shilingi 886,000,000 ambayo katika ya hiyo ni ya ujenzi wa vyumba 25 vya madarasa ambapo jumla ya vyumba 55 vya madarasa vitafanyiwa ukarafati ili viweze kutumika katika hali nzuri

Alisema halmashauri yake imepanga kujenga nyumba 12 mpya za walimu na kukarabati nyingine 12 za walimu ambapo ujenzi wa nyumba mpya utagharimu kiasi cha shilingi 250,000,000 na ukarabati utagharimu kiasi cha shilingi 48,000,000 pamoja na kumalizia ujenzi wa nyumba 10 za walimu zilizoanza kujengwa na ujenzi wake kukwama kutokana na sababu mbali mbali ikiwamo ukosefu wa fedha.

Kwa kauli moja baraza hilo la madiwani lililoongozwa na mwenyekiti wake, Mhe. Wilbroad Mayala, lilipitisha bajeti hiyo na kusisitiza fedha hizo kuletwa kwa wakati kutoka hazina ili ziweze kuanza kutumika kulingana na mpango kazi wake pamoja na kuepusha tatizo sugu la miradi viporo linalosababishwa na kupanda kwa gharama za manunuzi.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top