WAKATI binadamu wakiendelea na mipango yao ya kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kimazingira, kiulinzi na usalama, utabiri mpya wa kutisha unaonesha kuwa mwaka 2032 ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu katika mfumo wa jua.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao ya internet, sayari
iitwayo Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo njiani
kuigonga dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.
Kwa mujibu wa mitandao hiyo ya kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea dunia kwa kasi kubwa, itaonekana kubwa na angavu wakati wa usiku angani na kuwa katika umbo la mwezi na hivyo kufanya miezi ionekane miwili.
Taarifa zaidi za kisayansi zinasema kuwa, kadiri sayari hiyo inavyozidi kusogea, dunia itaanza kutikisika na kusababisha matetemeko ya ardhi kuongezeka sehemu mbalimbali.Mbali na dunia kutikisika na matetemeko, milipuko ya volcano nayo itatokea huku idadi kubwa ya milipuko hiyo mipya ikiongezeka, vimbunga vikubwa kama Tsunami vitaibuka na mwishowe dunia itapigwa na bomu la miamba midogo na vimondo kutokea angani.
Wakati volcano zote duniani zitakapoanza kulipuka na zingine mpya kujitokeza, dunia itafunikwa na giza nene na matope kwa wakati wote wa usiku na mchana huku watu wakitakiwa kusoma katika Biblia Joel 2: 1-2 na Zephaniah 1:14-17.
Nibiru inatajwa kama kitu kinachoisogelea dunia kinachoaminiwa kusababisha madhara makubwa ambapo kama hakitaigonga dunia, kitasababisha mtikisiko usio wa kawaida kitakapopishana nayo. Baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kitendo hicho kitatokea mapema katika karne ya 21 (tuliyonayo sasa).
Baadhi ya wanasayansi wanapinga kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wowote wa kitafiti unaoonesha wazi kwa mabingwa wa anga za juu waliobobea wa masuala ya nyota.
Kwa mara ya kwanza jambo hilo lilitokea mwaka 1995, wakati mwanamama Nancy Lieder muasisi wa mtandao wa ZetaTalk, aliwahi kudai kuoteshwa ndoto kwamba, Mei 2003 kuna kitu kitaingilia mfumo wa jua (solar system) na kusababisha dunia kutoboka tundu litakalosambaratisha sehemu kubwa ya kizazi cha binadamu.
Lieder aliifafanua kuwa, kitu hicho kitakuwa na ukubwa wa mara nne ya dunia.
Baada ya mwanamama Lieder, mtu wa
kwanza kuizungumzia Nibiru alikuwa Mark Hazlewood, mwanachama wa zamani
wa mtandao wa ZetaTalk ambaye mwaka 2001 alichapisha kitabu kilichoitwa
Blindsided na kusema kuwa mwisho wa dunia ungekuwa mwaka 2003 baada ya
kuwasili kwa sayari ya kumi (Nibiru).
Katika mfumo wa sasa, baadhi ya wanasayansi wanasema sayari ziko 12,
wakizitaja kwa namba 1. Jua 2. Mercury 3. Venus 4. Dunia 5. Luna (mwezi)
6. Mars 7. Jupiter 8. Saturn 9. Uranus 10. Neptune 11. Pluto 12.
Nibiru.
Hata
hivyo, utabiri mpya uliotolewa na watu wa jamii ya Vikings jijini New
York, Marekani umesema mwisho wa dunia ni Februari 22, mwaka huu.
Mitandao mbalimbali pamoja na gazeti maarufu la Daily Mail la
Uingereza lilielezea utabiri huo uliofanywa na jamii hiyo ukidai kuwa
mwisho wa dunia utatokana na Mungu Odin kupigana na kuuawa na shetani
Wolf Fenrir, hivyo kuiachia dunia anayoishikilia.
Wamesema baada ya kuiachia dunia itafurika maji ambayo yatakuwa na sumu, hivyo viumbe wote watateketea.
Baadhi ya watumishi
wa Mungu nchini wamekuwa wakisimamia andiko la kwenye Biblia linalosema
kuwa, hakuna mwanadamu anayeijua siku wala tarehe ya mwisho wa dunia na
ni siri ya Muumba.
Makanisa mengi nchini Tanzania yana sera tofauti lakini yanaongozwa
na Biblia moja. Makanisa hayo ni Romani Katoliki, Lutheran (KKKT),
Anglikana na makanisa ya kiroho kama Full Gospel& Bible Fellowship
la Zakaria Kakobe.
Jamii ya Freemason tayari imebariki mwisho wa dunia kwamba umefika na dunia inatarajie tukio kubwa la pamoja.
Mitandao ya jamii hiyo inataja kama hizi ni nyakati za mavuno kwa
maana kwamba, upande wa Mungu na shetani kushindania watu huku waendao
upotevuni wakiwa wengi.
Kwa mujibu wa kitabu
kinachoitwa Panorama ya Biblia, ulimwengu tangu kuumbwa kwake umekuwa
na matukio makubwa kila baada ya miaka 2000 (inaweza isitimie au ikapita
kidogo).
Tangu kuumbwa kwa Adamu na Eva mpaka gharika inadaiwa ni miaka 2000.
Gharika hadi dunia kubadili mfumo wa mawasiliano (Mnara wa Babeli) ni
miaka 2000. Kuzaliwa kwa Yesu hadi sasa ni miaka 2000 ambapo katika karne
hii, dunia huenda ikaingia katika tukio kubwa sana ambalo halijawahi
kutokea.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment