Wabunge nchini Uganda leo wanaanza kujadili hatua ya
serikali kuwapeleka bila idhini ya bunge wanajeshi wa taifa hilo nchini
Sudan Kusini.
Serikali iliamrisha wanajeshi hao kupelekwa Sudan Kusini kufuatia mapigano yaliyozuka huko Disemba mwaka jana.
Mjadala unatarajiwa kuwa mkali kwani baadhi ya wabunge wanahoji uhalali wa majeshi ya Uganda kuwepo nchini Sudan Kusini.
Jukumu la wanajeshi hao katika vita hivyo bado halijawekwa wazi kwa wabunge watakaopigia kura hoja hiyo.
Waziri wa ulinzi anatarajiwa kuhojiwa kuhusu
swala hilo kabla ya wabunge kupiga kura kuidhinisha wanajeshi hao
kushika doria Sudan Kusini.
Rais Yoweri Museveni alisikika akitoa vitisho
dhidi ya kiongozi wa waasi Riek Machar kuwa ikiwa hatasitisha vita
huenda akapeleka wanajeshi wa Uganda kwenda kusaidia majeshi ya serikali
ya Sudan Kusini kupambana na wapiganaji wake.
Museveni aliamrisha majeshi hayo kwenda Uganda
wakati wabunge walipokuwa likizoni, hali iliyosababisha malalamiko
kutoka kwa wabunge hao.
Jumanne waziri wa ulinzi atatakiwa kufafanua na
kutoa majibu kuhusu muda ambao wanajeshi wa Uganda wataendelea kusalia
Uganda pamoja na kutaka kujua kazi wanayoifanya huko.
Baadhi ya wabunge wamemtuhumu Rais Yoweri
Museveni kwa kwenda kinyume na katiba kwa kuwaamrisha wanajeshi wa nchi
kwenda Uganda kuwaokoa raia waliokuwa katika nchi hiyo inayokumbwa na
mgogoro wa kisiasa wakati vita vilipozuka.
Wabunge hao wanahoji Wanajeshi wa Uganda wako Sudan Kusini kwa mwaliko wa nani, ikiwa ni IGAD au AU wanataka kujua.
Wanaituhumu serikali kwa kukosa kutoa majibu kuhusu idadi ya wanajeshi wa UDF walio nchini humo wakihofu hali ya usalama.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment