Mkurugenzi wa Sahel Trading Co.Ltd, Ally hazam kushoto akimkabidhi mzani wa kupimia uzito mabondilla 'Ostadhi' mzani huo wenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nane umetolewa na kampuni hiyo kutekeleza ahadi yao ya kusaidia mchezo wa masumbwi nchini picha na www.superdboxingcoach.blogspot.coma kwa Yassin Abda |
MAZANI WA KIMATAIFA WA KUPIMIA MABONDIA AMBAPO UNA UWEZO WA KUPIMA
UZITO,UREFU, NA KUTAMBUA UJAZO WA MAFUTA YAKO MWILINI YAPO KIASI GANI NA
UNAITAJI UWE NA UZANI KIASI GANI KULINGANA NA UREFU WAKO
Mkurugenzi wa Sahel Trading Co.Ltd, Ally hazam kushoto
akimkabidhi mzani wa kupimia uzito mabondia kwa Yassin Abdalla 'Ostadhi'
mzani huo wenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nane umetolewa
na kampuni hiyo kutekeleza ahadi yao ya kusaidia mchezo wa masumbwi
nchini picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Sahel Trading Co.Ltd kupitia kwa mkurugenzi wake Ally
Hazam wametoa mzani wa kupimia mabondia kwa kiwango cha hali ya juu kwa
ajili ya kuondoa ubabaishaji wa upimaji uzito kwa mabondia
Akizungumza wakati wa kukabidhi mzani huo wenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nane Hazam amesema wameamua kutoa mzani wakitegemea ngumi ndio mchezo pekee ambao unaweza kuliletea sifa taifa kwa haraka zaidi. Naye Yassini Abdalla 'Ostadhi' aliyepokea mzani huo ambao utakuwa ukitumika kwa mabondia kupima uzito hususani katika mapambano ya kimataifa ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa mzani ahadi ambayo walikuwa nayo muda mrefu lakini leo 'jana' ndio wameitekeleza Siku zote dunia nzima cha kwanza kabla mabondia awajapanda ulingoni kwanza wanapima uzito na afya ndio mpambano una endelea. Bila uzani kujulikana hakuna ngumi maana mnaweza kupiganisha mabondia wenye uzani tofauti kitu ambacho akikubaliki dunia nzima Hivyo sina budi kuishukuru kampuni ya Sahel Trading Co. Ltd kwa kunipatia uzani huu. |
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment