Mkuu wa Jeshi la Polisi MbeyaDiwani Athuman
WILAYA YA MBARALI -AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 12.10.2013 MAJIRA YA SAA 17:30HRS HUKO MSWISWI WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA BARABARA YA MBEYA/IRINGA. GARI NO T.793 CDF AINA YA SUZUKI LIKIEDNESHWA NA DEREVA JOSHUA S/O BRUNO SANGA, MIAKA 41, MKINGA NA MKAZI WA MAKAMBAKO ALIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE FRANK S/O NGUKU,
MIAKA 45, MBENA, MKAZI WA MSWISWI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.
MWILI WA MAREHEMU UMEKABIDHIWA KWA NDUGU ZAKE KWA AJILI YA MAZISHI BAADA
YA KUFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI WA SERIKALI. CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA, TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA PIKIPIKI KUGONGANA NA
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.
MNAMO TAREHE 12.10.2013 MAJIRA YA SAA 22:30HRS HUKO MASHIWAWALA MBALIZI BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. PIPIKIPI NO. T. 908 CBC AINA YA SHINEY IKIENDESHWA NA DEREVA EMANUEL S/O NGAO, MIAKA 25, MNDALI, MKAZI WA MBALIZI ILIGONGANA NA PIKIPIKI NO. T 298 BZK AINA YA T/BETTER ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ATUPOKILE S/O ANGOLILE, MIAKA 34, MNYAKYUSA, MKAZI WA MBALIZI NA KUSABABISHA KIFO CHA MWARABU S/O ? ANAEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI 30-35 ALIYEKUWA ABIRIA KATIKA PIKIPIKI NO. T.298 BZK
NA KUSABABISHA MAJERAHA KWA MADEREVA WA PIKIPIKI HIZO. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMAHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA NA MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALINI HAPO. PIKIPIKI ZIPO
KITUONI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO
VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
0 comments:
Post a Comment