TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kama mnavyofahamu, Serikali  imeyafungia  magazeti ya Mtanzania na Mwananchi kwa kuzingatia  Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 na kanuni zake za mwaka 1977. Gazeti la Mwananchi limefungiwa kwa muda wa wiki mbili kuanzia tarehe 27 Septemba, 2013 na Gazeti la Mtanzania limefungiwa kwa muda wa miezi mitatu au siku 90 kuanzia tarehe 27 Septemba, 2013.

Aidha tunataka umma ufahamu kuwa Serikali  haikukurupuka  kufungia magazeti hayo. Uamuzi huo ulifanyika baada ya
kufuata taratibu zote za msingi ikiwemo kuwasikiliza wahusika.

Hata hivyo, tumeona gazeti la Mwananchi baada ya kufungiwa limeendelea kuchapishwa kwenye mtandao wa Internet kinyume cha amri  iliyotolewa. Kufanya hivyo ni kosa na  Serikali  tumewaandikia kuacha mara moja la sivyo, Serikali italazimika kuchukua hatua kali zaidi.

Aidha kampuni ya New Habari 2006 baada ya kufungiwa moja ya magazeti yake, imeanza  kuchapisha gazeti la ‘Rai’ kila siku tangu tarehe 29 Septemba mwaka 2013 bila ya kibali cha Msajili wa Magazeti. Hilo nalo ni kosa,  Serikali  inawataka kuacha mara moja kuchapisha gazeti hilo kila siku na warudie ratiba yao ya kuchapisha mara moja kwa wiki mpaka hapo maamuzi mengine yatakapofanyika.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI –MAELEZO
TAREHE   1/10/2013

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top