Serikali ya Afrika Kusini imesema kuwa rais wa
zamani wa nchi hiyo, Nelson Mandela, ametolewa hospitali ambako amekuwa akitibiwa
mapafu tangu mwezi wa Juni.
Taarifa katika tovuti ya rais wa Afrika Kusini
imeeleza kuwa Bwana Mandela bado ni mahtuti na hali yake wakati mwingine
inabadilika.
Lakini madaktari wake wanaamini akiwa nyumbani kwake mjini Johannesburg atapata matibabu sawa na yale ya hospitali.
Nyumba ya Bwana Mandela imebadilishwa ili kumruhusu kupata matibabu ya mgonjwa mahtuti akiwa nyumbani.
Serikali imesema inamtakia mema wakati akiendelea na matibabu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment